Kiswahili

Historia ya The Baobab Home na mpangilio wa shughuri zake  

The Baobab Home ilianzishwa mwaka 2004 kwa jitihada za pamoja za mume na mke, Caito Mwandu na Terri Place. Baobab ipo Bagamoyo, Tanzania. Baobab pia imesajiliwa kama taasisi ya kimataifa isiyo ya kiserikali ndani ya Tanzania. Kamati ya kuratibu ya watu wanaojitolea imechunguza uasilia wa Baobab, kisheria na mipango ya kifedha na kuthibitisha taratibu za utekelezaji wake kisheria. The Baobab Home pia inaushirikiano na jimbo la New Jersey ambapo pia imesajiliwa kama taasisi ya kusaidia wenye uhitaji. Mnamo mwaka 2008, Baobab ilipata msaada kutoka kutoka kwa watu wa jimbo la Califonia. Msaada huo uliweza kusaidia kugharamikia ununuzi wa shamba lenye heka zipatazo 10 lililopo umbali wa kilometa 5 kutoka Bagamoyo mjini. Tunatumia nishati ya jua (solar power) na gesi itokanayo na vinyesi vya wanyama kwa matumizi ya kupikia na shughuri nyinginezo.

Michakato yetu ya kijamii

Japokuwa jina la The Baobab Home limekuwa likitumika mara kwa mara kama nyumba ya watoto, ambayo ilifunguliwa mwaka 2008, lakini Baobab imekwenda mbali zaidi ya mtazamo huo. The Baobab Home inashughurika pia na w atoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu (yaani watoto wenye uhitaji), watu walioathirika na vvu na wanaoishi katika hali ya umasikini ndani ya Bagamoyo. Ni kwa miaka 9 tangu tulipoitikia kufanya mabadiliko ya kimahitaji kwa tatizo la HIV/AIDS kwa kuanzisha michakato mbalimbali ili kusaidia mahitaji ya msingi kama vile, chakula, shule na makazi, michakato yetu ni kama ifuatavyo.

Nyumba ya watoto: The Baobab Home ilifungua milango yake kwa watoto yatima na wale wote waliokosa msaada kutoka kwenye familia zao mnamo tarehe 24/12/2008. Tumelenga kuimarisha mahusiano ya watoto na familia zao na wale wasio yatima na watoto wetu. Kumekuwa na tabia watoto kutengwa/kutopata msaada au hakuna ndugu wa familia aliye teyari kuishi na mtoto aliye yatima, hata kama watoto hao wanapata msaada kutoka nje ya familia zao. Baobab ni mahali watoto hao ukaribishwa na kupewa upendo,lishe bora ,elimu ,matibabu na hakuna ubaguzi wa aina yoyote hata kama motto ni muathirika wa vvu. Tangu hapo tulikuwa na watoto ishirini tulioishi nao hapa Baobab, watoto kumi kati yao wengine walilithishwa na wengine waliunganishwa na familia zao, mnamo mwaka 2010 tilimpoteza mtoto mmoja aliyefariki duinia kwa tatizo la vvu. Kwa sasa tunaishi na watoto kumi.

Mchakato wa chai: Tangu mwezi wa 8 mwaka 2005 Baobab imekuwa ikitoa huduma ya kifungua kinywa kwa watoto wapatao 200,000 ambao miongoni mwao ni wanafunzi wa shule za kawaida (shule za serikali) na watoto wenye vvu. Mchakato huu ulianza kwa watoto wa shule za kawaida ambapo walipatiwa huduma ya uji, huduma hii ilitolewa kwa watoto kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu (wenye uhitaji) wa Bagamoyo (MVC). Mchakato huu pia ulitupatia nafasi ya kuweza kuwaangazia watoto na kutambua ishara za matatizo yao nyumbani mwao, ishara hizo ni kama vile kupungua kwa uzito, kuumia na kupotelewa kwa sare zao za shule. Mnamo mwaka 2009 mchakato wa kifungua kinywa (uji) ulisogea mpaka katika kliniki ya utoaji huduma na matibabu kwa wagonjwa wa vvu ambapo tulitoa huduma ya uji kwa wagonjwa wa vvu zaidi ya 1000 kwa kila mwezi kwa kutoa huduma hii ya lishe kwa wagonjwa, kwa wale wote walio tokea mbali paka kufikia kliniki, tumelenga kuwaongezea nishati zao na utayari wao kuweza kusikiliza madaktari wanasema nini kwa kufika kliniki mara moja kila mwezi, huo ni muda ambao wanatakiwa watazamie hasa kujifunza jinsi ya kujari afya zao na jinsi ya kuzuia maambukizi ya vvu.

Stronger Together: Kwa makadilio karibia watoto 160,000 ambao wanapata matibabu ya vvu hapa Tanzania. Lakini idadi ya walio athirika ni mara tatu ya idadi iliyo hapo juu Baobab ina amini kuwa watoto hawa wanazo haki lakini wamekuwa wakizaraurika na kuachwa, hali hii inapelekea watoto hawa kuangaika. Kwa witikio wetu tumeanzisha kikundi cha watoto wenye vvu ambacho huendeshwa mara mbili kwa wiki hapa Bagamoyo. Kikundi hiki kina shughuri mbalimbali ambazo watoto hushiriki kwa pamoja kama vile, ngoma, kuogelea, kufanya shughuri nyingine za kisanii, na kufanya vikao ambapo watoto hujadili mambo mbalimbali kuhusu tatizo la vvu na matokeo yake kwa ujumla. Tumeunda kikundi cha watu wa kujitolea kutoka nje kwa ajiri ya kusaidia kuendesha shughuri na kulipia chakula na matunda katika kili mkutano.

Steven Tito Academy: Baobab imejitoa kuhakikisha kwamba umasikini usifanye watoto kukosa elimu wanayostahili kuhipata kama haki yao kimsingi. Steven Tito Academy (STA) ni iliyofunguliwa kwa ajiri ya kusaidia watoto wenye uhitaji, ni shule ya msingi ya kiingereza iliyopo katika shamba letu. Ni shule yenye madarasa yenye umbo dogo kwa ajiri ya kuweka mazingira mazuri na ya muda mrefu ili kila mtoto apate mafunzo bora ili aje awe kiongozi bora. STA ina bustani na yenye ushawishi ili watoto waweke jitihada katika kujifunza elimu ya mazingira na sayansi.

Do you like this page?

The Baobab Home Nonprofit Overview and Reviews on GreatNonprofits

Review The Baobab Home on Great Nonprofits

The Baobab Home Nonprofit Overview and Reviews on GreatNonprofits

Sign in with Facebook, Twitter or email.